


Julius Kambarage nyerere alizaliwa mnamo mwaka 1922 (Katika kijiji cha Butiama,Wilaya ya Musoma,Mkoa wa Mara,Tanzania (wakati ule:Tanganyika)Alikuwa mojawapo kati ya watoto 26 wa Nyerere Buriko,Chifu wa kabila la wazanaki.Alipokuwa Mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake,katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilometa 30 hadi Musoma.Baada ya kumaliza shule ya msingi,aliendelea kusoma shule ya Wamisionari Wakatoliki huko Tabora.Katika Umri wa miaka 20 alibatizwa akawa Mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma Ualimu huko Makerere,Kampala - Uganda,Kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha Tawi la umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na Tawi la Tanganyika African Association (TAA).Baada ya kumaliza masomo ya ualimu,alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary's. Mwaka 1949 alipata Skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma M.A ya historia na Uchumi (Alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Uingereza,na Mtanzania wa pili kupata Shahada ya elimu ya juu ya Tanzania)Aliporejea Tanganyika alipotoka masomoni,Nyerere alifundisha Historia,Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar - es - salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa Rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), Chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika Chuo kikuu cha Makerere.Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU),ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya Mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha kisiasa zaidi kinachoongoza Tanganyika.Uwepo wa Mwl. Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere achague kati ya Siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na Machifu ili kuleta Muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika TRUSTEESHIP COUNCIL na FOURTH COMMITTEE ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila kumwaga damu.Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa Gavana wa wakati huo bwana Richard Tumbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa Uhuru. Nyerere aliingia katika Bunge la kikoloni Mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 1960.Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake,na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliawa kuwa Waziri mkuu wa Tanganyika Huru na mwaka mmoja baadaye nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania,Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa Madarakani Sultani wa Zanzibar Jamshid Bin Abdallah. 05/02/1977 Mwl.Nyerere aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na Chama Tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi),Nyerere akiwa Mwenyekiti wake.Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi Mwaka 1985 alipomwachia nafasi Rais wa Pili Ali Hassani Mwinyi.Aliendelea kuongoza chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Inasadikika kuwa nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamin . W . Mkapa kama mgombea wa Rais wa mwaka 1995 na ambaye aliteuliwa kuwa Rais kwenye Uchaguzi wa mwaka 1995. Nyerere alikaa muda wake mwingi Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya aliyoyaanzisha taasisi yenye jina lake, Mwaka 1996 alionekana akiwa Mpatanishi wa pande Mbali mbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.Tarehe 14/10/1999 aliaga dunia katika hospitali ya St.Thomas London,Kwa ugonjwa wa kansa ya damuNdio maana kila Mwaka tarehe 14 mwezi wa 10 Serikali imetenga siku hii kuwa siku ya Kumbu kumbu Kitaifa kumuenzi Hayati Mwl.J.K.Nyerere.